﷽
THE REGISTERED TRUSTEES OF IMAMUL MUZANIY FOUNDATION
MARKAZIL IMAAMIL–MUZANIY
MUONGOZO WA MARKAZIL IMAAMIL –MUZANIY
Markazil Imaamil Muzaniy Foundation, iliopo mtaa wa Butiama kata ya Vingunguti Dar-es salaam, inafanya shughuli zake katika maeneo mbalimbali hapa Tanzania.
SHUGHULI ZA KIIBADA
Markaz husimamia shughuli zake kwa kuzingatia Qur-an na Sunnah na hilo hufanywa kwa kuhakikisha waumini wanakuwa katika mwenendo sahihi wa wema waliotangulia (Sallaf-Swaleh)
ELIMU
Markaz inajihusisha na kutoa Elimu kwa Waislam na jamii kwa ujumla kama ifuatavyo:
Kupitia Vituo
Kupitia Misikiti
Mihadhara ya nje
i/ Kupitia Vituo
Markaz hutoa Elimu kwa Waumini kwa kuwajenga wawe na tabia nzuri kuzingatia ujirani mwema Amani , Ushirikiano Uzalendo na mambo mengine yanayojenga Taifa letu
ii/ Kupitia Misikitini
Markaz hutembelea Misikiti mbalimbali ndani ya Dar es Salaam na Mikoa mingine ( nje ya Dar es Salaam) kwa ajili ya kuelimisha Waislam juu ya tabia njema ikiwemo kutaja umuhimu wa kuwa na Amani na Uzalendo katika Nchi.
iii/ Mihadhara ya nje
Markaz itatoa Elimu yake katika Viwanja vya nje pale itakapowezekana na hilo litafanyika kwa kuzingatia Sheria na nidhamu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
USAJILI WA WANAFUNZI
Markaz husajili Wanafunzi wake kama ifuatavyo:
( i) Wanafunzi wa Bweni (Boarding)
( ii) Wanafunzi wa kutwa (Day)
i/ Wanafunzi wa Bweni (Boarding)
Markaz husajili Wanafunzi wake kwa mwaka wasiozidi thelathini na tano (35).
Mwanafunzi anatakiwa awe amemaliza Darasa la saba na awe hana sifa ya kuendelea na Elimu ya Sekondari.
ii/ Wanafunzi wa kutwa (Day)
Markaz husajili Wanafunzi wa kutwa (Day) kama ifuatavyo;-
( i) Watoto wadogo (Madrasa)
( ii) Watu wazima
i/ Watoto wadogo (Madrasa)
Watoto hao wanasajiliwa waume kwa wake na hao wanaripoti Madrasa baada ya kutoka katika Elimu yao ya Mazingira.
ii/ Watu wazima
Markaz husajili watu wazima, wake kwa waume, pia wanatakiwa kuwa wamemaliza Darasa la saba na kushindwa au kufeli kuendelea na Elimu ya Sekondari
KIWANGO CHA ELIMU
Markaz hutoa kiwango cha Elimu ya awali- (IBTIDAAIYA)- na ya juu-(THANAWI) kwa watu wa Bweni na kutwa (Day and Boarding).
NAMNA YA UPOKEAJI WA MWANAFUNZI
Mwanafunzi anatakiwa kuripoti Markaz kwa masharti tajwa katika fomu ya kujiunga
ikiwemo barua ya Serikali ya mtaa ili kuweza kumjua kwa undani sehemu anakotoka.
7. UENDESHAJI WA MARKAZ
Markaz inaendesha shughuli zake za Kiibada na kutoa Elimu ya Dini kwa watu na jamii kwa ujumla, na hilo ni kuzingatia mambo yafuatayo;-
Markazi ina matawi yake katika baadhi ya mikoa hapa nchini yakiwa yanafanya kazi zake kama ilivyo ainishwa katika katiba yetu.